Sunday 14 June 2015




MCHANGANUO NA MAELEZO JUU YA UFAULU WA WANAFUNZI



Moja kati ya changamoto zinazowakumba wanafunzi wa kitanzania ni kuweza kupata matokeo yaliyo bora na ya kuridhisha, wanaamini kuwa ufaulu wao upo chini ya walimu wao kitu ambacho sio cha kweli, wanafunzi wa kileo hawtaki kuazana kusoma kwa bidii ,badala yake wanabaki wakicheza na mitandao ya kijamii kama vile facebook, twiter na watsap. Mwisho wa siku wanajikuta wanapoteza mda wao mwingi wa kujisomea ,matokeo yake ni kujitumbukiza katika mambo yasiyo maadili yetu.

Jamii yetu ya kitanzania inaendelea kukosa wataalamu kama vile wa afya,kilimo na uongozi, matoeo yake ni umasiini ulioithiri kulio kawaida, na kubwa zaidi ni kutokuendelea kwa taifa letu na Africa yetu wa ujumla.


Zifuatazo ni njia sahihi za mwanafunzi ataazofuata ili kuweza kupata matokeo yaliyo bora na sio bora matokeo,ni msimamo wangu kwamba endapo njia hizi zitazingatiwa vizuri wanafunzi wetu wanaweza wakafanya vizuri na kutuletea matunda mazuri kwa taifa letu;

  •  Majadiliano kwa vikundi juu ya mambo waliyojifunza darasani
  • kujitahidi kutafuta njia sahihi juu ya mada ambazo hazieleweki na sio kussubiri mwalimu kwa kila kitu.
  • Matumizi mazuri ya mda pamoja na kujipangia ratiba ya kujisomea mda wa nyumbani.
  • Na mwisho kabisa ni nidhamu bora pamoja na kuwatii wazazi wao ,hii itasaidia wazazi kuwapenda wanafunzi wao na hata kuwanunulia vifaa vya kujisomea, bila kusahau kufanya ibada umuomba mungu awasaidie.